Mhe Baba Askofu Charles Rabson Mjema akiwa katika Ibada Maalumu ya Kumstaafisha Mchungaji Elinkanileka Mlemba iliyofanyika Katika Usharika wa Tae Jimbo la Tambarare..
Ibada hiyo ilihudhuriwa na Wachungaji na Wakuu wa Majimbo kutoka Jimbo la Tambarare Mch. Itikija Kizinga, Jimbo la Mashariki Mch. Mkiramweni na Jimbo la Magharibi Mch. Greyson Mhale.
Mchungaji Elinkanileka ambaye katika Ibada hiyo alikuwa anastafu akiwa ametumika kwa Miaka 28 tangu awe Mchungaji na ametumika katika Sharika mbalimbali za Dayosisi ya Pare.