
Jimbo la Magharibi
Jimbo la Maghaibi ni mojawapo ya Majimbo matatu ya KKKT Dayosisi ya Pare kwa sehemu kubwa Jimbo linahudumu katika maeneo ya milimani mwa Wilaya ya Same. Jimbo lina jumla ya Sharika 13 na limegawanyika katika kanda 2; Kanda ya Magharibi ina Sharika za Vudee, Chome, Mhero, Tae, Suji na Ndowa. Kanda ya Kusini ina Sharika za Myamba, Ivuga, Bwambo, Kirangare, Mwala papa, Makasa na Ngarito
IDADI YA WASHARIKA
Kutokana na sensa iliyofanyika 2021, Jimbo lina Washarika 15,585 kati yao watoto ni 39% na watu wazima ni 61% Katika watu wazima wanaume ni 45% na wanawake ni 55%
Huduma Zetu
Katika Jimbo la Magharibi zipo huduma nyingine kando na huduma ya msingi ya kueneza Injili, huduma zitolewazo ni”
UDIAKONIA na HUDUMA ZA KIJAMII
- Jimbo kupitia Sharika zake limekuwa likitoa huduma kwa familia zenye mazingira hatarishi kwa kuwasaidiwa Mavazi na Chakula
- Mfuko wa Diakonia wa Jimbo ambao unatumika kusaidia watumishi wa Jimbo wanapopata misiba, au wagonjwa.
- Jimbo linatoa huduma kwa washokeri/wagonjwa kwa kuwatia moyo kwa Neno la Mungu, kuwapa Sakramenti na misaada mbalimbali ya kibinadamu.
HUDUMA ZA ELIMU
- Shule ya Awali Mwala papa: Ni shule inayowaandaa wanafunzi kabla ya kuandikishwa darasa la kwanza, Shule hii inaendeshwa na Usharika wa Mwala Papa
Viongozi wa Jimbo
Mch. Greyson Y. Mhale
Mkuu wa Jimbo
Mch. Mbazie Kirumbi
Msaidizi wa M/Jimbo
Bw. Elisafi Ngoye
Katibu