Mhe Baba Askofu Charles Rabson Mjema Tarehe 26 Januari 2025, ameshirikiana na Baba Askofu Dkt Msafiri Joseph Mbilu Mkuu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ambaye limwakilisha Mkuu wa Kanisa Katika Ibada Maalum ya Uzinduzi wa Mwaka wa Yubile ya Kuzaliwa kwa Dayosisi ya Pare, Ibada iliyofanyika katika Usharika wa Bombo na Ibada iliyoambatana na Kubariki wa Watheologia 3 kuwa wachungaji, Kustaafisha kwa Heshima wachungaji wawili ( Mch. E. Sengoro na Mch. Peter Fue), Kustaafisha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Dayosisi na Kuingiza Kazini wajumbe wengine wapya wa Halmashauri Kuu ya Dayosisi, Sambamba na Matukio hayo Makubwa katika Ibada hii pia Baba Askofu Dkt. Msafiri Mbilu aliweza kuizinduia Tarehe rasmi mwaka wa Maazimisho pamoja na Siku ya Pare Day.
Tarehe 16/03/1975 Dayosisi ya Pare ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ilzinduliwa rasmi na kusimikwa viongozi wake wa Kwanza Mchungaji Eliewaha Elia Mshana, na Msaidizi wa Askofu Mchungaji Stefano Ombeni Msangi.