
Kuhusu sisi
KKKT Dayosisi ya Pare ni moja wapo ya Dayosisi 26 zilizo chini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. Hapo awali ilikuwa sehemu ya Kanisa la Kilutheri la Kaskazini mwa Tanganyika hadi 1963, na baadaye ikawa jimbo la Pare chini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini (KKKT ND) hadi mwaka wa 1975 ilipojitenga na Dayosisi ya Kaskazini na kusajiliwa rasmi kama Dayosisi ya Pare kwa usajili namba SO 5951 wa tarehe 30 -07-1975. ikiunganisha wilaya za Same na Mwanga. Mwaka 2016 Dayosisi ya Pare iligawanyika na kuzaliwa dayosisi ya Mwanga iliyopo wilaya ya Mwanga na Dayosisi ya Pare ikibakia ndani ya wilaya ya Same.
Eneo la Dayosisi la Pare limegawanywa katika maeneo matatu ya kiikolojia ambayo ni; eneo la nyanda za juu, Ukanda wa kati na ukanda za chini.
Ukanda wa nyanda za juu; Eneo hili liko kati ya mwinuko wa meta 1,100-2,462 juu ya usawa wa bahari likiwa na idadi kubwa ya watu inayofikia watu 650 kwa kilomita ya mraba. Ukanda huu unapata kiasi cha mvua kati ya milimitata 1250 hadi 2000 kwa mwaka. Joto huanzia nyuzijoto 15 –hadi 250 kwa kipimo cha centgrade. Mfumo wa makazi huathiriwa sana na hali ya kitopolojia ambapo watu hujenga nyumba katika mashamba yao. Ardhi ya kilimo katika eneo la juu inatumika kikamilifu ambapo kilimo ndio shughuli kuu ya kiuchumi ya watu. Ukanda wa juu zaidi umefunikwa na misitu ya asili.
Ukanda wa kati ,Eneo hili lipo kati ya mwinuko wa mita 900 – 1100 juu ya usawa wa bahari, pia lina idadi kubwa ya watu inayofikia watu 250 kwa kila kilomita ya mraba na hupata mvua kati ya 800 – 1250 mm kwa mwaka. Kiwango cha joto ni kati ya nyuzi joto 25 hadi 30 C
Ukanda wa chini (Tambarare) Ukanda huu upo kati ya mita 500 – 900 juu ya usawa wa bahari na hupata mvua kati ya 500 – 800 mm kwa mwaka. Ukanda huu ni nusu kame na unatawaliwa na wafugaji
Viongozi Wetu

Rev. Charles Mjema
Bishop
Rev. Ibrahim Ndekia
Assistance Bishop
Mwl.Tumaini Chambua
General Secretary
Mr. Daniel Msuya
Treasurer