
Jimbo la Mashariki
Jimbo la Mashariki ni mojawapo ya Majimbo matatu ya KKKT Dayosisi ya Pare kwa sehemu kubwa Jimbo linahudumu katika maeneneo ya milimani mwa Wilaya ya Same. Jimbo lina jumla ya Sharika 11 na limegawanyika katika kanda 2; Kanda ya Mashariki ina Sharika za Mtii, Ngaeni, Bombo, Mramba na Ntenga Kanda ya Maghaibi ina Sharika za Msindo, Mbaga, Mbwakweni, Marindi, Mhezi na Mwembe.
Huduma Zetu
Katika Jimbo la Mashariki zipo huduma nyingine kando na huduma ya msingi ya kueneza Injili, huduma zitolewazo ni”
UDIAKONIA na HUDUMA ZA KIJAMII
- Jimbo kupitia Sharika zake limekuwa likitoa huduma kwa familia zenye mazingira hatarishi kwa kuwasaidiwa Mavazi na Chakula
- Mfuko wa Diakonia wa Jimbo ambao unatumika kusaidia watumishi wa Jimbo wanapopata misiba, au wagonjwa.
- Jimbo linatoa huduma kwa washokeri/wagonjwa kwa kuwatia moyo kwa Neno la Mungu, kuwapa Sakramenti na misaada mbalimbali ya kibinadamu.
HUDUMA ZA ELIMU
- Shule ya Awali Bombo: Ni shule inayowaandaa wanafunzi kabla ya kuandikishwa darasa la kwanza, Shule hii inaendeshwa na Usharika wa Bombo
Viongozi wa Jimbo
Mch. Enirisha Mkiramweni
Mkuu wa Jimbo
Mch. David Tendwa
Msaidizi wa M/Jimbo
Bw. Christopher Kilonzo
Katibu