Skip to content

Jimbo la Tambarare


Jimbo la Tambarare ni mojawapo ya Majimbo matatu ya KKKT Dayosisi ya Pare kwa sehemu kubwa Jimbo linahudumu katika maeneneo ya Tambarare  ya Wilaya ya Same. Jimbo lina jumla ya Sharika 15 na limegawanyika katika kanda 2;  Kanda ya Mashariki ina Sharika za Kisiwani, Maore, Ndungu na Kihurio.   Kanda ya Magharibi ina Sharika za Kizungo, Same, Kanisa Kuu, Kisima, Ebenezer, Makanya, Hedaru, Agape, Ruvu, Kanani, na Bethlehemu.

Jimbo lina Sharika za Misioni ambazo ni Ruvu, Kanani, na Kizungo pia yapo baadhi ya maeneo ya Misioni katika Usharika wa Makanya ambayo ni Kinyangusi, Chankoko, Naivoli, Emau A, Emau B na Makei. Maeneo haya ni ya jamii ya wafugaji,

IDADI YA  WASHARIKA

Kutokana na sensa iliyofanyika 2021, Jimbo lina Washarika 27,190 kati yao watoto ni 12, 373 sawa na 45.5% na watu wazima ni 14,817 sawa na 54.5%. Katika watu wazima wanaume ni 48.3% na wanawake ni 51.7%.

Huduma Zetu

Katika Jimbo la Tambarare zipo huduma nyingine kando na huduma ya msingi ya kueneza Injili, huduma zitolewazo ni”

UDIAKONIA na HUDUMA ZA KIJAMII

Tousled letterpre tote bag bicycle rights cliche twee hashtag pokpo demos tanero lamina sime voti. Wolf moon shoreditch biodiesel hoodie kale chips bitter

  • Jimbo kupitia Sharika zake limekuwa likitoa huduma kwa familia zenye mazingira hatarishi kwa kuwasaidiwa Mavazi, Chakula na gharama za matibabu; hata katika Hospitali ya rufaa KCMC.
  • Mfuko wa Diakonia wa Jimbo ambao unatumika kusaidia watumishi wa Jimbo  wanapopata misiba, au wagonjwa.
  • Huduma kwa wafungwa katika gereza  la Wilaya Same. Vifaa mbalimbali vinatolewaga kuhudumia wafungwa ambavyo ni; sabuni, ndala, dawa za meno, miswaki, Pedi, na mafuta.
  • Kwa Sasa Jimbo limewahudumia watumishi wastaafu 34 (wajane 8, Wainjilisti 21, na wachungaji 5) Kupitia Mfuko maalum wa Wasitaafu; 
  • Jimbo linatoa huduma kwa washokeri/wagonjwa kwa kuwatia moyo kwa Neno la Mungu, kuwapa Sakramenti na misaada mbalimbali ya kibinadamu.
  • Usharika wa Kanisa Kuu na Usharika wa Ruvu kuna Huduma ya Mtoto na Kijana ambapo watoto waishio katika mazingira hatarishi husaidiwa huduma za kiroho, kielimu, kiafya na kijamii.

HUDUMA ZA ELIMU

  • Shule ya Msingi na Awali ya Mkomazi: Shule hii ni Mpya imeanzishwa mwaka 2021 na ipo yalipo makao makuu ya Dayosisi. Shule hii ni ya Mchepuo wa Kiingereza na Inaendeshwa na Usharika wa Kanisa Kuu.
  • Shule ya Msingi na Awali St Andrews: Shule hii ni ya Mchepuo wa Kiingereza ipo Usharika wa Hedaru.
  • Shule ya Awali Makanya: Ni shule inayowaandaa wanafunzi kabla ya kuandikishwa darasa la kwanza, Shule hii inaendeshwa na Usharika wa Makanya.
  • Shule ya Awali na Chekechea Muungano. Hii ni Shule ya Kanisa inayoendeshwa na Usharika wa Ruvu.

Viongozi wa Jimbo

Mch. Itikija Kizigha

Mkuu wa Jimbo

Mch. Rose Mfuko

Msaidizi wa M/Jimbo

Mwj. Zephania Mghamba

Katibu